Kitaifa

Abdallah Juma, Pastory wapewa jukumu la kuinusuru Stand United

on

STAND United inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kutokana na washambuliaji wake kushindwa kufunga mabao ya ushindi hivyo sasa wameamua kuimarisha zaidi safu hiyo.

Mpaka sasa Stand United yenye maskani yake mjini Shinyanga imefanya usajili wake katika nafasi tofauti huku washambuliaji Pastory Athanas na Abdallah Juma wakiongezwa kikosini kuinasua timu hiyo.

Pastory ni kama amerudi nyumbani baada ya kushindwa kufanya vizuri katika klabu ya Simba alikokuwa amesajiliwa kabla ya kwenda Singida United kwa mkopo ambao nao hawajaona msaada wake huku Abdallah yeye akiwa mchezaji huru.

Uongozi wa Stand pamoja na benchi la ufundi wanaamini nyota hao wataisaidia timu yao ili isishuke daraja kwani wanaamini bado wana uwezo mkubwa wa kupambana.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Dr Ellyson Maeja amekiri kukamilisha mipango ya usajili kwa wachezaji hao.

“Pastory amerudi nyumbani na tunaamini kiwango chake bado ni kizuri, tumemsajili pia Abdallah Juma na wachezaji wengine ambao kocha alipendekeza,”. Alisema Dr. Maeja

Simba ilimsajili Pastory baada ya kung’aa katika mchezo dhidi ya Yanga Stand wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga huku straikabakifunga bao hilo pekee.

Singida wao waliamua kumsajili wakiamini atawasaidia ila ameshindwa kuonesha makali yoyote na hivyo kupelekea muda mwingi awe nje ya uwanja.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *