Burudani

Ali Kiba, Diamond Platnumz wadhihirisha ubabe wao Afrika Mashariki

on

Tanzania imeingia tena kwenye ‘headlines’ za vyombo mbalimbali vya habari za burudani Afrika Mashariki katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2018 baada ya wasanii wa nchini hapa kutisha kwenye shoo za nchi jirani.

Diamond Platnumz kutoka WCB ameuanza mwaka kwa kuweka historia nchini Kenya katika mji wa Naivasha kwenye onyesho ambalo msanii huyo amewashukuru sana wakenya kwa sapoti waliyompa hadi kufikia kutamka kuwa Kenya ni nchi yake ya pili baada ya Tanzania.

Diamond Platnumz akiwa jukwaani katika tamasha Naivasha-Kenya

Msanii kutoka Rockstar2000 Ali Kiba alifungua mwaka kwa kufanya maajabu katika jiji la Kigali nchini Rwanda. Mashabiki wengi sana walihudhuria shoo yake ikiwa ni ishara kwamba muziki wake unapendwa sana nchini humo.

Ali Kiba akiwa jukwaani

Upinzani mkubwa uliopo baina ya mashabiki wa Diamond ‘Team Diamond’ na wale wa Kiba ‘Team Kiba’ umeongeza chachu ya muziki wao na kuwafanya wasanii hao watoe kazi nzuri zilizowapa mafanikio makubwa sana ndani ya 2017 huku wakiuanza mwa 2018 kwa dalili njema za kutisha zaidi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *