Kimataifa

Arsenal walivyolazimika ‘kuilipa’ Chelsea ili wampate Aubameyang

on

YAMESALIA masaa machache dirisha la usajili barani Ulaya lifungwe ifikapo saa 5:59 usiku wa leo lakini katika siku hii ya mwisho uhamisho wa wachezaji watatu ndio umeteka hisia za wadau wengi wa soka hasa kutokana na mtindo wa duara uliotumika.

Straika wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang amekamilisha uhamisho wake kujiunga na Arsenal ambayo imemuuza Olivier Giroud kwa Chelsea iliyomwachia kwa mkopo Michy Batshuayi kwenda Dortmund.

Hatma ya washambuliaji hao wote watatu ilikuwa inategemeana huku uhamisho wa mkopo wa Batshuayi ukionekana kuwa ndio ulibeba funguo za mchakato mzima. Taarifa kutoka Ujerumani zinasema Arsenal walilazimika kuilipa Chelsea kiasi cha paundi 1.3 milioni zilizohitajiwa na Chelsea kama ada ya mkopo wa Mbelgiji huyo.

Batshuayi

Arsenal walilazimika kufanya hivyo ili tu kurahisisha ‘deal’ yao ya kumnasa Aubameyang ambaye alikuwa aking’ang’aniwa na Dortmund kwavile walikuwa hawajapa mbadala wake.

Kwa mantiki hiyo Dortmund wanakuwa hawajaingia gharama yoyote kumpata kinda huyo zaidi ya kumlipa mshahara wake wa kila wiki hadi mwishoni mwa msimu huu.

Wakati Chelsea wakimtoa Batshuayi kwa mkopo walikuwa tayari wameshajihakikishia saini ya Giroud kutoka Arsenal ambaye pengo lake linaenda kuzibwa na Aubameyang.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *