Kitaifa

ATUPELE: Sijaachwa Singida, nimeondoka

on

SIKU moja baada ya uongozi wa Singida United kutangaza kuachana na wachezaji wawili huku wengine wawili wakitolewa kwa mkopo, Atupele Green amefunguka kuwa si kweli kwamba ameachwa bali yeye ndiye aliomba kuvunja mkataba.

Atupele alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo iliyopanda daraja msimu uliopita lakini ameitumikia kwa miezi sita pekee na kuamua kukaa mezani na viongozi wake ili kuvunja mkataba huo ili kwenda kujaribu maisha sehemu nyingine.

Akizungumza na BOIPLUS, Atupele alisema kuwa sababu kubwa ni kukiukwa kwa baadhi ya makubaliano yao yaliyokuwemo kwenye mkataba wake ambapo uongozi ulishindwa kuyatekeleza.

Atupele (kushoto) akifanya mazoezi na kikosi cha Singida United kabla hajaachana na klabu hiyo

“Mimi ndiye niliyeomba kuvunja mkataba wangu baada ya kuona baadhi ya makubaliano hayatimizwi, hivyo nilitaka niwe huru kwenda kucheza sehemu nyingine.

“Kwasasa nipo katika mazungumzo na timu nyingine za ligi kuu hivyo mambo yakienda vizuri ndipo nitaweka wazi wapi nitacheza mzunguko wa pili,” alisema Atupele.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo aliushukuru uongozi wa Singida United kuwa wasikivu katika makubaliano yao na kukubali kuuvunja mkataba wake.

“Nawashukuru viongozi wangu walikuwa wasikivu katika hili, mchezaji unatakiwa kuheshimu mkataba wako, kufuata maagizo ya mkataba yanavyosema lakini pia mwajiri wako naye anapaswa kufuata mkataba ili kazi iende vizuri, ” alisema Atupele

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Isaya Mwaseba

Recommended for you

1 Comment

  1. kim da yu mbwana

    December 5, 2017 at 7:38 pm

    Atupele bana anatufanya vichaaa,kwani ukifukuzwa ni kwamba hujuh si vile tuu hauna nafasi au umeshindwa kufikia malengo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *