Kitaifa

Azam FC mabingwa kombe la Mapinduzi

on

AZAM FC wamefanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA kwa mikwaju ya penati 4-3, mechi hiyo ya fainali imechezwa usiku wa leo Jumamosi uwanja wa Amaan visiwani Unguja.

Azam na URA walitinga katika hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika mechi zao za awali huku URA wakishinda mechi zote walizocheza na Simba, Yanga pamoja na Azam FC.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 zikitoka sare tasa na hivyo kulazimika kuingia katika hatua ya matuta ambapo kila timu ilipiga penalti tano.

Azam FC wakishangilia ubingwa wao

Waliofunga penati kwa upande wa Azam ni Himid Mao, Yakubu Mohamed, Enock Atta na Aggrey Moris wakati Bruce Kangwa pekee akikosa.

Upande wa URA penati zao zilipigwa na Patrick Mboa, Brian Majegwa ambao walikosa huku Charles Sepa, Shafik Kajimu na Jimmy Kulaba wakipata.

Azam ambao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu kwa kuwa na pointi 26 watarejea jijini Dar es Salaam kesho Jumapili kuajiandaa na mechi ya ligi kuu dhidi ya Majimaji itakayochezwa Januari 18 uwanja wa Majimaji mjini Songea.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *