Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Azam mmemsikia kocha wa Majimaji?

0 338

KOCHA wa Majimaji FC Habibu Kondo amesema wanafahamu kuwa wapo mahali pabaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu lakini kazi ya kujinasua itaanza rasmi Ijumaa hii katika uwanja wa Azam Complex itakapokuwa ikipambana na ‘Wanalambalamba’ Azam FC.

Akizungumza na BOIPLUS kwa njia ya simu akiwa njiani na kikosi chake kuja jijini Dar es Salaa, kocha huyo amesema kwamba wanahitaji pointi tatu tu katika mchezo huo na mingine miwili inayofuata ili wasalie Ligi Kuu.

“Tunajua mechi za mwisho wa Ligi ni ngumu sana hasa hizi za ugenini lakini tumejipanga vizuri ili tuweze kushinda zote tatu zilizosalia kwani hiyo ndio nusura yetu.

Related Posts
1 of 18
Kocha wa Majimaji Habibu Kondo

“Kwakweli hatupo kwenye nafasi nzuri hivyo hatuna sababu ya kumfikiria mtu mwingine, tunapaswa kutazama mechi zetu tu na matokeo pekee tunayoyatafuta ni ushindi, tunashukuru wachezaji wote wapo vizuri hakuna majeruhi” alisema Kondo.

Timu hizo zilishindwa kutambiana zilipokutana kwa mara ya mwisho katika uwanja wa Majimaji mjini Songea baada ya kutoka sare ya bao moja na sasa zitakutana Mei 11 saa 1:00 usiku huko Chamazi katika mechi ya kumaliza ubishi.

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...