Burudani

Azam TV kuiamsha Bongo Movie kwa bonge la tamasha

on

KITUO cha runinga cha Azam kimezindua tamasha kubwa la filamu za Kiswahili ‘Sinema Zetu International Film Festival’ Afrika Mashariki litakaloshindanisha filamu za Kiswahili ambapo kileleni chake kitakuwa Aprili Mosi 2018.

Azam kupitia Chaneli namba 103 ya Sinema Zetu mahususi kwa ajili ya kuonyesha filamu za kitanzania ‘Bongo Movies’ itashindanisha filamu zaidi ya 150 za Kiswahuli kutoka ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Sinema zetu Jacob Joseph amesema nia ya tamasha hilo ni kurudisha heshima ya filamu za kitanzania ambayo inaonekana kushuka kwa sasa.

Jacob alisema wameweka vituo katika mikoa ya Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Mtwara. Pia kutakuwa na vituo katika miji ya Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura na Goma kwa ajili ya kukusanya filamu zitakazoshindanishwa kuanzia leo mpaka Novemba 31.

Mratibu wa tamasha, Zamaradi Nzowa (kulia) akieleza jambo katika mkutano wao na waandishi wa habari

“Tumeweka vituo kadhaa sehemu mbalimbali ili wadau wa filamu waweze kukusanya kazi zao kwa ajili ya tamasha hili, ni zile tu zilizochezwa kuanzia 2015 hadi 2017,” alisema Jacob.

Naye Mratibu wa tamasha hilo Zamaradi Nzowa amesema filamu zitakazoshindanishwa ni zile ndefu, fupi na makala huku zawadi zikienda kwa kila mshiriki.

“Zawadi zitatolewa kwa muigizaji bora wa kiume, wa kike, muongozaji bora, mpiga picha bora, mhariri bora, mchekeshaji bora, mwandishi bora wa mswada na mtengenezaji bora wa mziki wa filamu. Wote hao watapata zawadi za cheti na pesa taslimu kuanzia sh milioni tano,” alisema Nzowa.

Lulu

Elizabeth Michael ‘Lulu’

Kwa upande wake balozi wa tamasha hilo Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye pia ni muigizaji wa Bongo Movie alisema tamasha hilo litaongeza chachu kwa wadau wa filamu kutengeneza filamu bora na baada ya miaka mitatu tasnia hiyo itarejea kwenye ubora wake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *