Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Baada ya kutishiwa kichapo, Simba wasema hawana hofu hata kidogo

Wapitia ubani Bungeni kwa ajili kwenda kubeba ndoo Singida

0 579

BAADA ya kocha msaidizi wa Singida United Jumanne Chale kujigamba kwamba Simba hawawezi kupata pointi nyumbani kwao, Meneja wa Wekundu hao wa Msimbazi Robert Richard amesema wao hawana presha yoyote kwani wanauchukulia mchezo huo kama mingine iliyopita.

Jana kocha huyo alizungumza na mtandao huu na kuwaonya Simba wasitarajie kutangaza ubingwa kwenye uwanja wao, jambo ambalo limejibiwa na Meneja huyo kuwa wanajua mechi ya kesho wanajua ndiyo ya Ubingwa kwao.

“Sisi tuko vizuri hatuna wasiwasi hata kidogo, kila mmoja wetu anajua mchezo wa Jumamosi ni muhimu sana kwetu kwamba ndio mechi yetu ya ubingwa hiyo.

Related Posts
1 of 18

“Lakini pia sisi tuna malengo ya kumaliza ligi bila kupoteza mchezo kwahiyo uzito tulioweka kwenye michezo iliyopita tutaendelea nao mpaka ligi itakapomalizika,” alisema Robert.

Katika hatua nyingine Robert amesema kikosi chao kimeondoka leo asubuhi kikipitia Dodoma walikoalikwa na wabunge mashabiki wa timu hiyo.

“Tumeondoka leo asubuhi lakini tunapitia Dodoma tulipoalikwa na waheshimiwa Wabunge, tutalala pale halafu kesho tutaendelea na safari ya kuelekea Singida.”

Simba wanaenda Singida kutafuta pointi ushindi ili watwae ubingwa wa msimu huu huku Singida wakitaka kulipiza kisasi cha kutandikwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza jijini Dar.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...