Burudani

Bongo Movie wazindua kampuni yao, Mwakyembe awapa tahadhari wamachinga

on

JIONI ya Jumamosi Disemba 2, wasanii wa filamu za Bongo maarufu kama ‘Bongo Movie’ wamezindua kampuni yao ya kusambaza na kusimamia kazi zao inayoitwa Barazani Entertaiment huku makao makuu yake yake yakiwa Kinondoni Studio jijini Dar esSalaam.

Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo alikua ni Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harison Mwakyembe ambaye aliwaahidi wasanii hao kwamba serikali itashirikiana nao kwa nguvu zote.

“Moja ya changamoto kubwa iliyochangia kurudi nyuma kwa tasnia hii ya filamu ni mitaji, nina imani ujio wa kampuni hii itakua njia ya kurudisha juu soko la filamu zetu, lakini pia Barazani nimkombozi wa wasanii wote naamini wengi watanufaika kupitia kampuni hii.” Alisema Mwakyembe.

Lakini pia Dk Mwakyembe akawatumia salamu wamachinga wote wanaouza DVD mitaani kwamba wajiandae ‘kufa’ kwa njaa kwasababu Barazani wanafanya kazi zote.

“Nawapongeza sana waanzilishi wa kampuni hii lakini pia nawaambia wauza DVD mitaani wajiandae kufa kwa njaa, hatutawakimbiza na mgambo lakini hawatapata tena DVD zetu,” alisema Mwakyembe.

Wasanii waliohudhuria kwenye shughuli hiyo ni Richie Mtambalike, Monalisa, Jackline Wolper, Natasha, Jimmy Mafufu, Jb ambaye ni Meneja masoko na uzalishaji na wengine wengi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *