Kitaifa

Bosi Big Bon, wanachama Simba watoa ya moyoni kuhusu mabadiliko

on

MWANACHAMA wa klabu ya Simba, Khalid Al-Tamim mwenye kadi namba 02621 amepongeza maamuzi ya wanachama wa klabu hiyo kukubaliana kwa pamoja kuingia kwenye mfumo mpya wa mabadiliko ya uendeshaji ambapo sasa itakuwa kampuni.

Mwishoni mwa wiki iliyopita wanachama zaidi ya 13,000 wa klabu hiyo waliridhia kuingia kwenye mfumo wa Hisa baada ya mfanyabiashara na mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kushinda zabuni ya uwekezaji kwa Sh 20 bilioni akiwa mwekezaji pekee aliyepeleka maombi yake katika Kamati ya Zabuni iliyoteuliwa na klabu hiyo.

Al-Tamim ambaye ni miongoni wa mabosi wa kampuni ya Mafuta ya Big Bon idara ya utunzaji kumbukumbu alisema kuwa amewahi kupata bahati ya kuzungumza na tajiri huyo ambaye aliwatoa hofu wanachama wanaofikiria kuwa Mo atawanyima haki yao.

Khalid Al-Tamim akizungumza na BOIPLUS

“Mo hana nia mbaya na Simba na amewahikishia wanasimba kuwa hii Simba itajengwa na kila mmoja na si peke yake, hivyo ni jambo jema kila mwanachama ana haki ndani ya Simba.

“Kitendo kilichofanywa na klabu yangu ni cha historia katika soka letu kuliko kuishi kwa kutegemea wadhamini pekee kwani mpira unahitaji pesa nyingi, kikubwa wachezaji watambue thamani ya Simba na kuheshimu ‘brand’ ya Simba, ” alisema Al-Tamim

Mwanachama mwingine aliyepata nafasi ya kutoa maoni ni Geoffrey Enock Shimwela ‘Geff’ wa tawi la Simba Damu Fans (SDF) Tabata mwenye kadi namba 8379 ambaye alisema tatizo kubwa lililochelewesha kufanikisha jambo hilo ni elimu juu ya mfumo wa hisa.

Mwanachama wa Simba, Geoffrey Shimwela

“Tunawapongeza viongozi wetu kwa kupambana kutoa elimu hadi kufanikisha jambo hili tena tukiwa na wenzetu ambao walikuwa wakilipinga, uelewa mdogo kuhusu hisa ndio uliofanya zoezi lichelewe,” alisema Geff.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa tawi la Mpira Pesa, Ustadh Masoud alisema, “Hakuna mwanachama anayechukia mabadiliko ndani ya simba tatizo lilikua jinsi mchakato ulivyo kuwa unaendeshwa, tunashukuru tumepewa elimu ya kutosha kila mtu ameridhika, nawashauri wanachama wenzangu na viongozi wangu waendelee kudumisha umoja kama kama kauli mbiu yetu inavyosema Simba nguvu moja,”

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *