Kitaifa

Si Tetesi Tena, Hii Hapa Habari Kamili ya Manji Kujiuzulu Yanga

on

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Yusuf Manji ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka mitano ambapo sasa Makamu wake Clement Sanga atakaimu hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Mapema asubuhi ya leo kulitoka taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu Mwenyekiti huyo kuachia ngazi ambapo barua iliyokuwa imetiwa saini na Manji ilianza kuzagaa kabla ya yeye mwenyewe kutangaza rasmi.

Manji amethibitisha hayo wakati akizungumza na kituo cha Radio cha EFM katika kipindi cha Sports Headquarter muda mfupi uliopita kuwa kwa sasa atakuwa mwanachama wa kawaida baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda huo.

“Hizo taarifa ni za ukweli na barua niliyo andika imejitosheleza sina haja ya kuongeza kitu,” alisema Manji.

Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Juni 12 mwaka jana Manji alichaguliwa kwa awamu ya pili ambapo amebakisha miaka mitatu kukamilisha muda wake uliobaki madarakani.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *