Burudani

BREAKING NEWS: Lulu atupwa jela miaka miwili

on

MAHAKAMA kuu nchini Tanzania imemtia hatiani msanii wa maigizo Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo iliyozua simanzi kubwa mahakamani hapo imesomwa muda mfupi uliopita baada ya mawakili wa Lulu kupewa nafasi ya kumtetea.

Lulu alimuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba ambaye ilielezwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Wakili wa muigizaji huyo Peter Kibatala, amesema watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *