Afrika

BREAKING: Zimbabwe wajitoa Chalenji kwa kuhofia usalama

on

SHIRIKISHO la kabumbu nchini Zimbabwe (ZIFA) limetangaza kujiondoa kwa timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la Chalenji inayotarajiwa kufanyika nchini Kenya hivi karibuni.

Taarifa ya ZIFA imesema sababu kubwa ya kujiondoa huko ni kutotengamaa kwa hali ya kiusalama nchini Kenya kufuatia mgogoro wa kiasiasa unaoendelea.

“Kujiondoa kwetu katika mashindano haya mazuri ni bahati mbaya kwetu, timu, taifa na waandaji kwa ujumla, lakini shirikisho ni lazima lifanye maamuzi sahihi kwa manufaa ya wengi.

“Tumesitisha maandalizi yote yaliyokuwa yakiendelea, lakini tunaahidi kushiriki michuano yoyote tutakayoalikwa siku zijazo ilimradi tu mazingira yawe rafiki,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo ZIFA imewaomba radhi waandaaji, wadhamini, timu shiriki, mashabiki na wadau kwa ujumla kutokana na usumbufu wowote uliojitokeza kufuatia maamuzi yao ya ghafla.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *