Kitaifa

Buswita kuanza na Njombe Mji baada ya kutoka ‘jela’

on

Mwandishi wetu
SIKU moja baada ya kuachiwa huru kiungo Pius Buswita amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 26 wa Yanga kitakachosafiri kesho asubuhi kuelekea mkoani Njombe kwa ajili ya mechi mbili za nyanda za juu Kusini dhidi ya Njombe Mji na Majimaji FC.

Buswita alifungiwa kutocheza kwa mwaka mmoja kutokana na kusaini timu mbili za Simba na Yanga ambapo jana Kamati ya Sheria, Katiba na hadhi za wachezaji ya TFF iliamuru nyota huyo kurejesha sh 10 milioni kwa Simba ili kuruhusiwa kucheza.

Kiungo huyo wa zamani wa Mbao FC aliukosa mchezo wa kwanza wa ligi wa mabingwa hao uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Agosti 27.

Mbali na Buswita wachezaji Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya nao wamejumuishwa katika kikosi hicho baada ya kuwa majeruhi tangu katika kipindi cha maandalizi ya ligi.

Kikosi kamili cha Yanga kitakachosafiri kesho kwa ajili ya michezo hiyo ni makipa Youthe Rostand na Ramadhan Kabwili. Walinzi ni Gadiel Michael, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Kelvin Yondan, Juma Abdul, Nadir Haroub, Hajji Mwinyi, Andrew Vincent, Hassan Kessy na Pato Ngonyani.

Viungo ni Papy Tshishimbi, Thaban Kamusoko, Buswita, Juma Mahadhi, Maka Edward, Mwashiuya, Raphael Daud, Said Juma, Said Mussa, Emmanuel Martin, Ibrahim Ajib na Yusuph Mhilu.

Washambuliaji ni Donald Ngoma, Matheo Anthony na Chirwa.

Yanga itaendelea kukosa huduma ya mshambuliaji wake nyota Amissi Tambwe, mlinda mlango Beno Kakolanya na kiungo Baruan Yahya ambao ni majeruhi na hawatasafiri na timu.

Mabingwa hao watashuka uwanjani siku ya Jumapili kucheza na Njombe Mji katika dimba la Sabasaba kabla ya kusafiri hadi mkoani Ruvuma kucheza na Majimaji Septemba 16 mjini Songea.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *