Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

CANAVARO: Mashabiki njooni uwanjani bila wasiwasi

0 307

NAHODHA wa Yanga Nadir Haroub ‘Canavaro’ amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwaambia waje uwanjani kwasababu watawapa furaha kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Canavaro alisema wanajua mchezo utakuwa mgumu lakini watajitahidi kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwasababu mashindano hayo ya Kimataifa ndio pekee waliyonayo hivyo watajitahidi wafike mbali. (Story inaendelea chini ya matangazo)

Related Posts
1 of 18

“Tumejiandaa vizuri tunajua tunaenda kukutana na timu nzuri ambayo ni mabingwa kwao lakini tumejipanga kupata ushindi hata wa goli moja ili tujiweke kwenye nafasi nzuri, tunaomba watanzania waje uwanjani kutusapoti,” alisema Canavaro.

Yanga inakutana na Rayon kesho kuanzia saa 1 usiku katika mchezo Wa pili wa hatua ya makundi utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar.

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...