Kitaifa

Chirwa arejea na mkosi, Yanga ‘Out’ URA fainali Mapinduzi

on

STRAIKA wa Yanga Obrey Chirwa ameingia visiwani Zanzibar asubuhi ya leo na kujumuishwa kwenye kikosi kilichotolewa na URA kwenye nusu fainali ya kombe la Mapinduzi huku yeye pekee ndiye akikosa mkwaju wa penati.

Chirwa aliyeingia dakika 53 kuchukua nafasi ya Pius Buswita hakuonyesha kiwango bora kwa dakika zote 37 alizocheza huku akionekana wazi kuwa mwili wake haukuwa sawa kimazoezi hali iliyojidhihirisha hata kwenye mkwaju dhaifu wa penati aliyoipeleka mikononi mwa kipa wa URA.

Yanga na URA zilishambuliana kwa zamu kwa karibu dakika zote za mchezo huku kila timu ikionekana kuwa makini zaidi kwenye safu ya ulinzi hali iliyopelekea timu hizo zimalize dakika 90 zikiwa hazijafungana.

Obrey Chirwa

Kwenye mikwaju ya penati ndipo URA ilifunga zote tano huku Yanga wakifunga nne na kupoteza moja pekee iliyopigwa na Chirwa ikiwa ni penati ya mwisho iliyoipa tiketi URA kwenda fainali.

Chirwa alikuwa nchini kwao Zambia kwa majuma kadhaa huku taarifa zikidai alikuwa kwenye mgomo baridi wa kushinikiza alipwe pesa zake usajili zilizosalia.

URA watasubiri mshindi kati ya Azam FC na Singida United zinazotarajiwa kupambana kuanzia saa 2:15 usiku huu kwenye dimba hilo hilo la Amaan.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *