Burudani

CHRISTIAN BELLA: Naitamani ‘nyota’ ya King Kikii

on

MUIMBAJI wa muziki wa dansi nchini Christian Bella ‘Mzee wa Masauti’ amesema anajivunia kuwa na kazi nzuri zisizoisha ladha kama ilivyo kwa wimbo wa ‘Kitambaa Cheupe’ ulioimbwa na mkongwe King Kikii.

Bella alisema kuwa, anatamani kazi zake ziendelee kuwa nembo yake katika miaka yote, kama ulivyo wimbo huo wa nguli wa muziki Kingi Kikii ambao ukipigwa sehemu yoyote ni lazima watu wainuke na kuucheza.

King Kikii akitumbuiza wimbo wake wa Kitambaa Cheupe

“Najivunia sana maisha yangu ya muziki toka analogi mpaka sasa digitali hivyo najua milima na mabonde yote katika muziki,” alisema.

Bella alisema katika maisha yake ya muziki anapenda kukosolewa iwe vibaya au vizuri kwani ili kufikia mafanikio ni lazima upitie changamoto hizo .

“Kuna wasanii hawataki kukosolewa kabisa. Mfano mtu anaandika kitu mtandaoni watu wakimkosoa anawatukana, sio vizuri unatakiwa kuwajibu vizuri na kujitafakari kwa nini wauponde wimbo hata kama wewe unauona mzuri,” alisema Bella.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *