Kitaifa

Cowbell waongeza ugumu mechi ya Yanga

on

KITENDO cha kampuni ya uzalisha na uuzaji wa maziwa ya Cowbell kumwaga mamilioni ya udhamini katika klabu ya Mbao leo kimeongeza chachu kwenye maandalizi ya mechi ya wakali hao wa jiji la Mwanza dhidi ya Yanga.

Cowbell ambao walianza kuidhamini Mbao tangu msimu uliopita, wameongeza mkataba leo hii kukiwa na maboresho kadhaa huku thamani ya mkataba huo ikitajwa kuwa ni sh 100 milioni.

Katika mkataba huo Mbao watakabidhiwa pesa taslimu sh 70 milioni huku sh 30 milioni zikitolewa kwa njia ya vifaa.

Mbao itavaana na Yanga Jumapili hii Disemba 31 hivyo kuingia kwa mamilioni hayo kutarahisisha maandalizi yao ikiwa ni pamoja na kupandisha morali ya wachezaji.

Katika makabidhiano hayo mwakilishi wa Cowbell, Elisalia Ndeta alisema wameamua kuwadhamini tena baada ya kuona waliyatumia vizuri mamilioni waliyowapatia msimu uliopita.

“Tumeamua kuendelea kuwadhamini kwavile hawakutuangusha msimu uliopita, walizitendea haki pesa tulizowapatia,” alisema Ndeta.

Naye Solly Njashi ambaye ni mwenyekiti wa klabu hiyo aliyasihi makampuni mengine yaendelea kujitokeza kutoa udhamini kwani gharama za uendeshaji wa timu zimekuwa kubwa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *