Burudani

‘Dawa’ yamuumiza kichwa Nini

on

MWANADADA anayeibukia katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Agnes Anthony ‘Nini’ amekiri kutotegemea mapokezi makubwa aliyoyapata tangu wimbo wake mpya wa ‘Niwe Dawa’ kutoka.

Msanii huyu anayefanya kazi kwa sasa na nyota wa muziki huo Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ au Mr. Nay kama anavyojitambulisha sasa anasema, hajaamini jinsi walivyompokea katika wimbo huo, kitu kinachomfanya azidi kuumiza kichwa jinsi ya kutoka.

Aidha Nini alisema, ni faraja kwake kwa kuwa anachipukia katika muziki hivyo ana imani atafanya vizuri kutokana na kukubalika kwa mashabiki wake.

Msanii Nini akihojiwa na mtangazaji wa BOIPLUS TV, Isaya Mwaseba


“Wimbo wangu wa Niwe dawa umetoka siku sio nyingi lakini cha kumshukuru Mungu umekubalika sana, na mimi nafurahi kwa kweli, nitazidi kuumiza kichwa ili niwaletee vitu vizuri zaidi,”

Msanii huyo mbali ya kudaiwa kutoka kimapenzi na Nay alikanusha vikali na kusema kuwa wanafanya kazi tu na hawana mahusiano ya aina yoyote lakini akiacha utata kwa kauli yake ya “labda kama itatokea hapo baadae” hali inayoashiria kuna jambo linaendelea baina yao.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Isaya Mwaseba

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *