Burudani

Diamond, Davido wang’ara Tuzo za Soundcity MVP 2017

on

MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameendelea kutisha na kuchanja mbuga kwenye muziki wa kimataifa akitangazwa kama mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka usiku wa Januari 12.

Diamond alitangazwa mshindi wa Tuzo za ‘Soundcity MVP Awards 2017’  katika kipengele cha Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka huku staa kutoka Nigeria Davido akiibuka na ushindi wa kishindo kwa kunyakua Tuzo tatu katika vipengele vya  wimbo bora wa mwaka ‘If’, video bora ya mwaka ‘If’ na mwanamuziki bora wa Afrika wa Mwaka.
Washindi wengine katika tuzo hizo na vipengele walivyoshinda ni kama ifuatavyo;

Painkiller- Sarkodie Ft Runtown wimbo bora wa kushirikisha

Maleek Berry-Msanii bora Chipukuzi wa Mwaka

Wizkid- Msanii bora kidigitali wa Afrika wa Mwaka

Distruction Boys-Kundi bora la mwaka

Wo-Olamide Chaguo la wasikilizaji

Mad Over You-Runtown, Chaguo la watazamaji

Casper Nyovest-Msanii bora wa ‘Hip Hop’

Maleek Berry-Msanii bora wa ‘Pop’

Young John-Muandaaji bora wa muziki 

If-Davido, wimbo bora

If-Davido, Video bora

Tiwa Savage-Msanii bora wa kike

Diamond Platnumz-Msanii bora wa kiume.

Tuzo hii kwa Diamond anayejiandaa kuzindua kituo chake cha redio na runinga hivi karibuni ni ishara kuwa muziki wa Bongo Flava unazidi kupaa kimataifa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *