Kimataifa

Drogba alivyohitimisha miaka 17 ya nywele zake

on

KIJANA aliyezaliwa mwaka 2000 sasa ana umri wa miaka 17 na kama aliendelea na masomo yake bila kukwama basi sasa anaweza kuwa amemaliza elimu ya sekondari kidato cha nne mwaka huu.

Kijana huyo anafanana umri na nywele za straika ‘lejendari’ wa Ivory Coast, Didier Drogba ambaye hapo jana aliamua kuzinyoa akihitaji kuwa mpya.

Mara ya mwisho kwa nyota huyo mwenye heshima kubwa katika klabu ya Chelsea kunyoa nywele zake ilikuwa ni Disemba 15, 2000 na jana zilikiwa zikitimiza miaka 17 kamili kabla hajaingia saluni na kuzikatisha ‘uhai’ wake.

Licha ya kuwa na umri wa miaka 39, mkongwe huyo bado ana nguvu na anaendelea kutisha kwenye ligi kuu nchini Marekani akiwa tegemeo katika klabu ya Phoenix Rising.

Drogba anayetarajia kustaa hivi karibuni aliifungia Chelsea jumla ya mabao 164 katika vipindi viwili alivyoichezea timu hiyo ya Uingereza.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *