Burudani

Enock Bella aibukia Wasafi

on

MSANII wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Enock Bella aliyewahi kutamba na kundi la ‘Yamoto Band’ anatarajia kuachia ngoma  mpya na msanii kutoka WCB Rayvanny hivi karibuni.

Bella anayefanya vizuri na kazi zake mbili alizoziacha mara baada ya kundi lao kusambaratika ‘Sauda’ na ‘Nitazoea’ aliyasema hayo jana wakati akizungumza na BOIPLUS kuhusiana na mipango yake baada ya nyimbo hizo kupokelewa vizuri na mashabiki wake .

‘’Nilipanga kuachia ngoma tatu kabla ya mwaka 2017 kuisha, lakini kutokana na mambo kuingiliana nikachelewa kuzitoa kazi hizo ndio maana mwaka huu mapema nikaitoa ‘Nitazoea’ lakini nategemea Februari kuachia kibao kingine’’

Msanii huyo alizungumzia pia utofauti uliopo wakati akiwa kwenye kundi la Yamoto na sasa yuko mwenyewe.

‘’Changamoto zipo maana kipindi kile kwenye kundi ilikuwa ni rahisi kusaidiana, kama kuna mahojiano mmoja akipata udhuru  wengine wanaenda, lakini kwa sasa hivi ukiangalia sina mtu yeyote anayenisimamia kwahiyo kila kitu nasimamia mwenyewe’’

Bella alivuma zaidi katika tasnia hiyo, kutokana na unogeshaji wake wa nyimbo kwa kutumia sauti yake nzito iliyoweza kumfanya ajulikane zaidi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Isaya Mwaseba

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *