Kimataifa

GUARDIOLA: Hatuna ujanja wa kubeba makombe manne

on

BAADA ya jana Manchester City kuibamiza Leicester City kwa penati 4-3 na kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Carabao, wadau wa soka wameanza kuitabiria makubwa timu hiyo kuwa inaweza kubeba makombe manne msimu huu.

Lakini unajua kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola amesemaje?, amekiri hawana ujanja huo na watu wasitarajie City kufanya maajabu ya aina hiyo msimu huu.

City walitangulia kwa bao la Bernardo Silva lakini Leicester wakalazimisha kwenda muda wa nyongeza baada ya bao la dakika ya mwisho la penati ya Jamie Vardy kwenye uwanja King Power.

City pia wapo pointi 11 zaidi ya anayemfuatia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini humo lakini Guardiola bado haamini wanaweza kushinda kila taji.

Pep Guardiola

“Haitokuja kutokea, hapana, sio sahihi, hiki kinachofikiriwa hakina uhalisia,

“Kubeba mataji yote tunayoshiriki si kitu cha kawaida, katika soka kuna kupoteza pointi na kuondolewa mashindanoni. Sifikirii nitatwaa mataji mangapi, nafikiria mchezo unaofuata,” alisema Guardiola katika mahojiano na televisheni ya Sky Sports.

City inashiriki ligi kuu nchini Uingereza, kombe la Carabao, Ligi ya mabingwa Ulaya na kombe la FA.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *