Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Hivi hawa mashabiki wa Simba watakaa wapi?

0 1,013

NDILO swali analoweza kujiuliza mtu ambaye alishaingia ndani ya uwanja wa Namfua hapa Singida majira ya saa 6 mchana kisha akatoka nje kutazama msururu wa mashabiki wanaohitaji kuingia ndani.

Uwanja huo ulifunguliwa mapema asubuhi na hadi muda huu majukwaa ya mzunguko na VIP yaliyoandaliwa kwa ajili ya mashabiki wa Simba yameshajaa wakati yale ya wenyeji Singida United yakiwa na nafasi tele.

Jukwaa la mzunguko la Simba linavyoonekana kutokea VIP
Jukwaa la mzunguko la Singida United kama linavyoonekana kutokea VIP

Wenyeji wameandaa utaratibu wa kugawanya majukwaa ili kila timu iingize mashabiki kulingana na ukubwa wa jukwaa lao jambo ambalo linaweza kuzua sintofahamu kama busara haitotumika kwani tayari mashabiki wengi wa Simba wana tiketi mikononi  na haieleweki watakaa wapi.

Related Posts
1 of 18
Jukwaa limeshajaa na kuna foleni ya kupanda jukwaani
VIP ya Singida bado inapumua
VIP ya Simba imebakiza nafasi chache tena ambazo ni za kulazimisha, si rasmi.
Na hivi ndivyo hali ilivyo nje ya uwanja

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...