Afrika

Hivi ndivyo mtoto wa Lwandamina alivyojimaliza kwa sumu

on

MTOTO wa kocha wa Yanga, George Lwandamina, Mofya ambaye taarifa za kifo chake zilisambaa mwishoni mwa wiki iliyopita amethibitika kuwa alijiua jijini Lusaka baada ya kujaribu kumuua binti wa miaka 25.

Mofya, 28, aliyekuwa akiishi maeneo ya Libala akiwa na mwenzake Keith Chemu, 16, walimfunga kamba binti huyo kabla ya kumpiga na kumbaka ambapo baadae alikutwa akiwa na majeraha shingoni na kifuani.

Msemaji wa jeshi la Polisi, Esther Katongo alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 mchana wa Ijumaa ya wiki iliyopita huku pia vijana hao wakimuibia binti huyo pesa kiasi cha Kwacha 400 na simu aina ya Samsung.

Bi. Katongo alisema baada ya tukio hilo Mofya aliamua kujiua kwa kunywa sumu huku mwenzake Keith akishikiliwa na jeshi hilo ambapo majeruhi anaendelea na matibabu katika hospitali ya UTH (University Teaching Hospitals) iliyopo Lusaka.

Kocha Oswald Mutapa Jr wa timu ya National Assembly ambayo hivi karibuni ilipanda ligi kuu (FAZ/MTN Super League) nchini humo alithibitisha kuwa mtoto huyo wa Lwandamina alikuwa mchezaji wake.

CHANZO: Mtandao wa Times, Zambia

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *