Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Juma Abdul aiangushia ‘Jumba Bovu’ ratiba ya Ligi

0 656

BEKI wa Yanga Juma Abdul amesema kwamba ratiba ya Ligi Kuu imechangia kuwanyima ubingwa wa msimu huu kwavile iliwabana sana.

Akizungumza na Azam TV mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons, beki huyo amedai kuwa uchovu wa safari ya kutoka Algeria umewafanya wasicheze vizuri leo huku kubana kwa ratiba yao kutokana na kukabiliwa na michuano ya kimataifa kumedhoofisha harakati zao kutetea ubingwa wao.

“Namshukuru mwenyezi Mungu tumemaliza mechi salama pia niwapongeze wapinzani wetu kwa ushindi.
Tumerudi Algeria hatujapumzika pia tumesafiri kuja Mbeya kwa basi, siku mbili kabla hatukufanya hata mazoezi.

Related Posts
1 of 18

“Najisikia vibaya sana sisi kama Yanga tushazoea kushika makombe pamoja na kucheza mashindano ya kimataifa. Tumepoteza makombe yote mawili FA pamoja na hili la Ligi Kuu, viongozi waangalie tumekosea wapi ili mwakani tuweze kufanya vizuri,” alisema Juma.

Yanga imevuliwa ubingwa rasmi baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Prison mabao yaliyofungwa na Eliuter Mpepo dakika 58 kwa njia ya penati huku la pili likifungwa na Salum Bosco dakika ya 85.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...