Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kagera ndani ya Dar tayari kutibua sherehe ya Simba

0 359

KOCHA mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema kwamba timu yake imeshawasili jijini Dar na wapo tayari kuwakabili Simba Jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa.

Akizungumza na BOIPLUS kwa njia ya simu kocha huyo amesema kuwa timu yake imejianda vizuri kwa ajili ya mchezo huo na hakuna walichobakiza kufanya katika kampeni yao ya kuibuka na pointi tatu.

Related Posts
1 of 18
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime

“Timu ipo Dar tayari na tumeshakamilisha maandalizi yote kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba, mpira ni dakika 90 hivyo baada ya hapo ndio tutajua inakuaje lakini tunamshukuru Mungu wachezaji wetu wote wapo vizuri hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri.”

Kagera ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi baada ya kujikusanyia pointi 31 ambazo haziwezi kufikiwa na yeyote katika timu tatu zilizo mkiani. Mchezo huo utakaotumika kuwakabidhi Simba kombe lao utaanza saa 8:00 mchana.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...