Kitaifa

BREAKING: Kaseke, Kenny wasamehewa Singida United

on

WACHEZAJI wa Singida United, Kenny Ally na Deus Kaseke wamesamehewa adhabu yao ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana na sasa wametakiwa kurejea kikosini.

Wachezaji hao walisimamishwa kwa utovu wa nidhamu lakini baadaye waliandika barua za kuomba msamaha barua ambazo Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahiman Sima alikiri kuzipokea.

Uongozi wa Singida United baada ya kupitia barua hizo umeamua kuwasamehe wachezaji hao na kuwataka kuripoti kambini ambapo watajiunga na kambi hiyo siku yoyote kuanzia sasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *