Burudani

Kauli ya Christian Bella kuhusiana na tuhuma za madawa ya kulevya

on

MSANII wa muziki wa dansi Christian Bella ‘Mzee wa Masauti’ amewataka wanaomchafua kuacha mara moja kwani katika maisha yake hajawai kujaribu kutumia madawa ya kulevya.

Akizungumza na BOIPLUS leo, Bella aisema anawashangaa sana, watu wanaotaka kumshusha kimuziki kwa kumpakazia mambo mabaya ambayo hajawahi kujaribu kuyafanya katika maisha yake.

“Unajua mimi siwezi kumzuia mtu asiongee, na katika maisha yangu ya sanaa huwa sipendi kujibizana na watu, lakini katika hili nimeona niliongelee tu maana linachafua taswira yangu,” alisema.

Bella alisema, anawajua hao wanaomchafua katika mitandao ya kijamii lakini hawezi kuwataja kwani wanajijua hivyo waache mara moja kwani yeye kipaji chake ni kutoka kwa Mungu na hakuna wa kumshusha.

“Hiyo skendo ni ya siku nyingi sana toka 2008, mtu kaamua tu maana kwenye mitandao ya kijamii ni sehemu ambayo huwezi kumzuia mtu kufanya anachokitaka, ila sijawahi kutumia aina yoyote ya dawa za kulevya na sina mpango huo,” alisema.

Aliongeza kwa kuwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani muziki ndiyo kazi yake kubwa aliyoichagua na inaendesha maisha yake, hivyo wasubiri burudani tu.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *