Kitaifa

Kichuya, Mkude na kocha wao kuhojiwa Simba

on

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba inatarajia kuwahoji wachezaji wake Jonas Mkude, Shiza Kichuya na Nicholaus Gyan kwa kitendo cha kutokaa benchi baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya URA.

Nyota hao wamezua sintofahamu kubwa miungoni mwa mashabiki wa klabu hiyo na mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo hicho ambacho kimeashiria utovu wa nidhamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Rais wa Klabu hiyo Salim Abdallah alisema hata wao viongozi hawakupendezwa na  kitendo kilichofanywa na wachezaji hao, hivyo watawaita na kuzungumza nao kwanza.

Alisema mara baada ya kusikiliza utetezi wao watamhoji kocha wao Masoud Djuma pia ili wajue nini kiini cha tukio hilo hadi nyota hao kugomea kukaa benchi mara tu baada ya kutolewa.

Kichuya akiwa jukwaani baada ya kufanyiwa mabafdliko

“Simba ni taasisi kubwa, ina kanuni na mfumo wake, tumeona walichokifanya, lakini kama uongozi makini tutawaita na kuzungumza nao na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya kama uongozi,” alisema.

Aidha Abdallah alisema, Simba haiungi mkono utovu wa nidhamu ndani ya timu na endapo itabainika walifanya makosa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa juu yao.

Hata hivyo kocha Djuma alizungumza na BOIPLUS mara baada ya mchezo wao dhidi ya URA na kukiri kuwa yeye ndiye aliyewaruhusu nyota hao wasikae kwenye benchi badala yake wakafanyiwe ‘massage’ chumbani.

Wakati huo huo kikosi cha Wekundu hao kinatarajia kuanza mazoezi rasmi kesho tayari kwa maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Clezencia Tryphone

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *