Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kimenya aeleza kinachomuumiza kuikosa Yanga leo

0 640

MCHEZAJI kiraka wa timu ya Tanzania Prisons Salum Kimenya amesema amesononeka sana kuukosa mchezo wao wa leo jioni dhidi ya mabingwa wa tetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga kwasababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Akizungumza na mtandao huu wa BOIPLUS Kimenya alisema inamuuma sana kukosa mchezo huo wa kihistoria kwavile alijiwekea malengo yake kwamba msimu huu asikose mchezo hata mmoja.

“Inaniuma sana kuwakosa Yanga kwasababu ni mchezo wa kihistoria kwetu tunaweza tukawavua ubingwa kama tukiwafunga, lakini pia nilikua na malengo yangu kwamba msimu huu nisikose mchezo hata mmoja, sasa naona imeshindikana.”alisema

Salum Kimenya (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Prisons bao
Related Posts
1 of 18

Kwa upande mwingine beki huyo ambae msimu huu ametumika zaidi kama kiungo mshambuliaji amesema pamoja na kukosekana kwake kwenye mchezo huo anaamini wachezaji wenzake watapambana na pointi tatu zitabaki Mbeya.

“Mimi sitakuwepo kwenye mchezo huo lakini naamini wenzangu hawataniangusha, mpira una matokeo ya kikatili sana hilo wenzangu wanalitambua na hawatawadharau Yanga, naamini pointi tatu zinabaki Mbeya,” alisema Kimenya.

Yanga wanashuka uwanjani kuzisaka pointi tatu ambapo wakifanikiwa watazidi kuuchelewesha ubingwa wa Simba ambayo inashuka dimbani Jumamosi hii dhidi ya Singida wakitafuta pointi mbili tu ili waweze kutwaa ubingwa wa msimu huu.

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...