Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kipa Ruvu Shooting anywa Mafuta ya taa

0 1,438

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida golikipa wa timu soka ya Ruvu Shooting Abdallah Rashid amenusuriwa na madaktari baada ya kunywa mafuta taa yaliyokuwa yamewekwa jirani na lango lake.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za Ruvu na Stand United.

Related Posts
1 of 18
Nyota wa Ruvu Shooting wakichuana na wa Stand United

Kadhia hiyo imetokea mara baada ya wasimamizi wa uwanja kupeleka mafuta ya taa langoni kwa Ruvu kwa lengo la kuyamwaga ili kufukuza siafu waliokuwa wamejazana uwanjani hapo na kuleta usumbufu kwa kipa huyo.

Rashidi alikunywa maziwa hayo akidhani ni maji ya kunywa, hata hivyo madaktari walimnusuru kwa kumpatia maziwa na maji.

Mchezo huo umeisha kwa Ruvu kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja lililofungwa na Rajab Zahir.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...