Kitaifa

KOCHA MASOUD: Niliwaruhusu Kichuya, Mkude kuondoka benchi

on

KAIMU kocha mkuu wa Simba, Masoud Djuma amewatetea wachezaji wake watatu kuwa wana nidhamu kubwa na yeye ndiye aliyetoa ruhusa kwamba wasikae kwenye benchi la ufundi baada ya kufanyiwa mabadiliko.

Katika mechi yao dhidi ya URA iliyochezwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, Djuma aliwatoa Shiza Kichuya, Nicholous Gyan, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto nafasi zao zilichukuliwa na Mohamed Ibrahim, James Kotei, Yusuph Mlipili, Laudit Mavugo na Said Ndemla.

Hata hivyo Simba imetolewa kwenye michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na URA bao 1-0 na hivyo kushika nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na pointi 4.

Baada ya wachezaji hao kuonekana kutokaa kwenye benchi la ufundi baada ya mabadiliko hayo wadau mbalimbali walitafsiri kwamba wachezaji hao wameonyesha utovu wa nidhamu kwa madai kuwa huenda hawakupenda kutolewa uwanjani.

Akizungumza na BOIPLUS Djuma amefafanua hilo kwamba, “Sio utovu wa nidhamu mimi ndiye niliyewaruhusu, hivyo hakuna tatizo lolote, walionekana kuchoka nikaruhusu wafanyiwe ‘masage’ huko huko chumbani, haikuwa na ulazima wao kurudi kukaa kwenye benchi tena, watu wasitafsiri vibaya,” alisema Djuma.

Akizungumzia mechi hiyo alisema kuwa, “Ni mechi ambayo ilikuwa na presha kubwa tulihitaji ushindi na wapinzani wetu walihitaji hilo, tumeondolewa mashindanoni hivyo tunapaswa kuangalia ligi kuu kuhakikisha tunafanya vyema,”.

Simba italazimika kurejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi za ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

 

Bofya picha hii hapa chini kujiunga nasi kwenye YouTube ndani ya BOIPLUS TV

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *