Kimataifa

Kocha wa Samatta apigwa chini Genk

on

Kocha Albert Stuivenberg aliyekuwa akiinoa KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta, ametimuliwa kazi muda mfupi uliopita kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Stuivenberg (47) ameitumikia klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji kwa kipindi cha mwaka mmoja huku msimu uliopita ikitisha kwenye ligi ya Europa ingawa ilishindwa kufuzu tena ikiwa mikononi mwake.

Genk iliyoonesha kukosa nguvu msimu huu chini ya mholanzi huyo ipo katika nafasi ya tisa ikiambulia pointi 23 pekee baada ya kushuka dimbani mara 18.

“KRC Genk inamshukuru Albert Stuivenberg kwa weledi na kujitoa kwake, tunamtakia kila la heri huko aendako,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya Jos Daerden akiisimamia katika mazoezi na mechi wakati uongozi ukiwa katika mchakato wa kutafuta kocha mpya.

Stuivenberg aliyezaliwa Rotterdam, Uholanzi alikuwa msaidizi wa Louis van Gaal katika klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka miwili. Kabla ya hapo alikuwa kocha wa vijana wa KNVB.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *