Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

LICHA YA KICHAPO: Rekodi za Barcelona zinatisha

0 81

MABINGWA wa Soka nchini Hispania, Barcelona usiku wa kuamkia jana walihitimishiwa safari yao ya kutopoteza mchezo baada ya kukubali kichapo cha mabao 5-4 toka kwa Levante.

Hata hivyo klabu hivyo imeweka historia kwa kuwa na takwimu za kustaajabisha msimu huu. Hizi hapa ni baadhi ya zinazowafanya wawe katika timu chache zilizofanya vizuri zaidi barani Ulaya msimu huu.

Wamecheza mechi 43 bila kupoteza
Wamejikusanyia jumla ya pointi 111
Related Posts
1 of 18
Ni siku 394 zilipita tangu wapoteze mechi kwa mara ya mwisho kabla hawajafungwa na Levante. Hii ni takribani mwaka mmoja na siku 28
Mpiga pasi bora ametokea kwao ambaye ni Ivan Rakitic aliyezitandika pasi 2732 msimu huu
Mkali Lionel Messi ameibuka mchezaji mwenye mabaomabaoengi zaidi (44) huku pia akiongoza kwa kutoa pasi nyingi zaidi za mabao (14) hivyo kuhusika katika upatikanaji wa mabao 58
Kikosi hicho kimefunga jumla ya mabao 122 msimu huu
Lakini wachezaji walioshiriki katika mafanikio hayo ni 29 tu

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...