Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Licha ya kuburuza mkia, bao la Samatta lawapa matumaini Genk Europa

0 872

KLABU ya KRC Genk ya Ubelgiji haijawa katika kiwango bora msimu huu na sasa inaburuza mkia katika mechi za ‘Play Off’ kuwania kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya pamoja na ligi ya Europa.

Bao la mtanzania Mbwana Samatta usiku wa Alhamisi liliwafanya waambulie pointi moja katika uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya bao moja na KAA Gent ingawa matokeo hayo hayakutosha kuwaondoa mkiani.

Akizungumza na BOIPLUS kwa njia ya simu, Samatta alisema sare hiyo inaweza kuonekana si kitu lakini kwa mipango waliyonayo imewasaidia kurahisisha mambo.

Related Posts
1 of 18

“Tumebakiwa na mechi mbili, tukishinda zote tutatoka nafasi ya mwisho na kupanda hadi namba nne ambapo tutapata nafasi ya kucheza mechi za awali za mtoano ligi ya Europa,” alisema Samatta.

Nahodha huyo wa Taifa Stars aliingia dakika 54 badala ya Nikos Karelis na kuisawazishia Genk hilo likiwa ni bao lake la tano msimu huu ambao ameshuka dimbani katika mechi 28 akicheza kwa jumla ya dakika 1647.

Genk itaikaribisha Sporting Charleroi Jumapili kabla hawajamaliza ligi kwa kuifuata Anderlecht Jumamosi ya Mei 19

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...