Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Licha ya kupata ajali, Alonso amaliza mbio

Asema angekuwa dereva mwingine angepaki gari.

0 59

Matairi mawili ya mbele yalipasuka na uvungu wa gari ukaharibika vibaya

BAADA ya kupata ajali mwanzoni mwa mbio za magari za Azerbaijan Grand Prix na kisha kuendelea, mkali wa Langalanga Fernando Alonso amesema anaamini kama ingekuwa dereva mwingine asingeendelea na mbio hizo.

Dereva huyo wa timu ya McLaren aligongwa na Williams wa Sergey Sirotkin mara baada ya kuanza mbio hizo hali iliyomlazimisha aendeshe hadi kwenye kituo cha ukarabati huku matairi mawili ya mbele yakiwa yametoboka.

Baada ya kubadili matairi hayo, Alonso aliendelea na mbio hizo na kufanikiwa kushika nafasi ya saba licha ya kuharibika vibaya kwa uvungu gari yake.

Baada ya mbio hizo Alonso alisema nafasi aliyomaliza ni matokeo ya ‘kukomaa’ kwake huku akiyataja kama matokeo bora zaidi katika maisha yake.

“Kali kuliko. Nafasi ya saba lakini iliyotokana na ustahimilivu wangu, naamini hakuna ambaye angeweza kumaliza mbio hizi, mimi ndiye wa kwanza wengine wangepaki magari yao.”

“Lakini sisi hatupaki wala kubadili gari badala yake tuliendelea kupambana kwenye kona zote tukinusurika kugonga kingo, nadhani ndio mashindano bora zaidi katika maisha yangu.”

Alonso aliongeza kuwa alipofika kwa mafundi na kubadilishiwa matairi walimweleza wazi wazi kuwa gari limeharibika sana hali iliyopelekea adhani aidha asingemaliza mbio au angelazimika kwenda mwendo wa taratibu sana.

“Licha ya matatizo hayo na taarifa ya mafundi kuwa gari limeharibika sana niliendelea na shindano nikianza kuyapita magari na kufanikiwa kumaliza katika nafasi hiyo.”

Stoffel Vandoorne ambaye yupo nae timu moja ya McLaren alimaliza shindano hilo akishika nafasi ya tisa.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...