Kitaifa

Licha ya kupigwa na Azam, hivi ndivyo Simba inavyotinga nusu fainali

on

HABARI ipo hivi…….Wekundu wa Msimbazi Simba waliingia kwenye dimba la Amaan usiku wa Jumamosi kwa lengo la kuwarejesha nyumbani Azam FC mapema zaidi. Lakini mambo yakawa kinyume, Wanalambalamba hao wakapata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Idd Kipagwile na kutinga nusu fainali.

Kama Azam wangepoteza basi Jumapili asubuhi boti ingewahusu kurejea Azam Complex Chamazi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi kuu ya Vodacom ikiwaacha Simba na URA zikitinga nusu fainali.

Baada ya matokeo ya leo, mashabiki wa Simba wameonekana kuchanganyikiwa wakiamini kuna nafasi finyu sana kwa timu yao kutinga nusu fainali hasa kwavile hata wakiifunga URA bado watafikisha pointi saba tu ambazo wakusanya kodi hao wa Uganda wanazo mkononi tayari.

Lakini hesabu ziko hivi, Azam anaongoza kundi kwa kujikusanyia pointi tisa akifuatiwa na URA wenye saba huku Simba wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi nne kibindoni. Kama Simba wataifunga URA maana yake watafanana nao pointi hivyo kuangaliwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

URA tayari ana tofauti ya +2 huku Simba akiwa na +1, hii ina maana Simba ikipata ushindi wa aina yoyote itakuwa na tofauti ya +2 au zaidi. Ikitokea ikawa +2 maana yake URA itapungua kuwa +1 au pungufu kwavile watakuwa wameruhusu mabao  na hapo ndipo Simba itatinga nusu fainali kiulaini kabisa.

Kwa mantiki hiyo Simba itaingia uwanjani kwa lengo la kusaka ushindi wa aina yoyote ili kuepuka kurejea nyumbani mapema huku URA wenyewe wakihitaji sare tu ili waungane na Azam kwenda nusu fainali.

 

Kutazama video za matukio mbalimbali ya MICHEZO na BURUDANI, tafadhali SUBSCRIBE kwenye chaneli yetu ya YouTube kwa jina la BOIPLUS TV…..Gusa hii picha chini itakupeleka

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *