Kimataifa

Maelezo, vikosi kuelekea Arsenal vs Liverpool

on

MACHO na masikio ya wadau wengi wa soka yameelekezwa katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza kati ya Arsenal na Liverpool unaotarajiwa kupigwa kwenye dimba la Emirates kuanzia saa 4:45 usiku wa leo.

Arsenal watamkosa straika wao Olivier Giroud kufuatia kuumia nyama za nyuma ya paja katika mchezo wa Jumanne wa robo fainali ya kombe la Carabao dhidi ya West Ham huku kukiwa na dalili za kukosa mechi zote za mwisho wa mwaka.

Francis Coquelin pia alitolewa katika mchezo huo akichechemea lakini bado anaweza kuwemo leo, Aaron Ramsey bado anaugulia maumivu huku pia Arsenal ikimkosa majeruhi wa muda mrefu, Santi Cazorla mwenye tatizo enka.

Kwa upande wa wageni, straika wao Daniel Sturridge na mlinzi Joel Matip wenye matatizo ya nyama za paja wapo kwenye hati hati ya kuwemo katika mchezo wa leo.

Alberto Moreno bado yupo nje kwa matatizo ya enka lakini Emre Can atakuwepo leo baada ya kukosekana katika mechi ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Bournemouth akitumikia adhabu ya kadi.

Alex Oxlade-Chamberlain leo atakutana na mabosi wake wa zamani

Adam Lallana ameandaliwa kuwemo kikosini tena baada ya kutokea benchi katika mchezo uliopita kwenye dimba la Vitality ukiwa ni mchezo wake wa pili msimu huu.

Wachezaji wa Arsenal wanaoweza kutumika leo ni: 
Cech, Ospina, Mertesacker, Holding, Mustafi, Koscielny, Chambers, Monreal, Debuchy, Bellerin, Nelson, Kolasinac, Maitland-Niles, Coquelin, Wilshere, Xhaka, Elneny, Ozil, Iwobi, Sanchez, Welbeck, Walcott, Lacazette.

Wachezaji wa Liverpool wanaoweza kutumika leo ni: 
Mignolet, Gomez, Lovren, Klavan, Robertson, Oxlade-Chamberlain, Henderson, Wijnaldum, Coutinho, Salah, Firmino, Karius, Alexander-Arnold, Milner, Can, Lallana, Mane, Solanke, Ings.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *