Burudani

Magari makali ya wasanii 6 wakubwa Tanzania

on

YAWEZEKANA hujawahi kupata nafasi ya kuona gari ya msanii ambaye ni kipenzi chako kutokana na umbali uliopo baina yenu, hii hapa ni orodha ya wasanii sita wakali na magari yao.

1. Diamond Platnumz


Bila shaka Diamond ni mmoja kati ya wasanii waliopata mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki. Alianzia chini kabisa hadi kupaa kimataifa huku akishirikisha na kushirikishwa na wasanii wakali wa Nigeria na Marekani.

Baada ya jitihada zote hizo, mkali huyo wa ‘Eneka’ na ‘Halellujah’ hajaacha kujizawadia mwenyewe kwa magari makali huku safari hii akivuta BMW X6 nyeusi inayokadiriwa kufikia thamani ya sh 200 milioni.

 

2. Ommy Dimpoz


Aliibuka na kujitambulisha zaidi mbele za mashabiki wa muziki kwa wimbo wa ‘Baadaye’, tangu hapo Ommy Dimpoz amekuwa akipambana bila kuchoka kuhakikisha muziki wake unapaa hadi kimataifa.

Kila mmoja anaweza kuona mafanikio yake kupitia magari anayoendesha. Ommy ni mpenzi wa Toyota ikishuhudiwa akitanua na Toyota Mark X kabla sasa hajavuta Toyota Prado ya kisasa.

 

3. Lady JayDee


Huyu ni mmoja wa wakongwe wa Bongo Flavour, amewahi kutisha na nyimbo kama ‘Ndi Ndi Ndi’ na ‘Yahaya’.

Ukikutana nae mtaani sasa atakuwa ndani ya Range Rover Evoque, unaweza usifanikiwe kumuona kutokana na vioo vya gari yake kuwa vya giza, lakini tambua tu kuwa yeye ni mmoja wa wasanii wa Tanzania wanaoendesha magari makali.

 

4. Wema Sepetu


Ni msanii anayetazamwa sana na jamii kwa kila kinachohusishwa na yeye bila kujali ni kweli au uongo, lakini cha uhakika ni kwamba Wema Sepetu ni mfanyabiashara makini sana.

Amefanikiwa kuingia kwenye tasnia ya burudani akitisha katika filamu kadhaa zinazomfanya awe juu, lakini kwenye ‘ishu’ ya magari, Wema naye hayuko nyuma, amewahi kumiliki Nissan Murano, Audi Q7 na Range Rover Sport ya 2015.

 

5. Ali Kiba


Kutokea Kigoma, ‘Cinderella’ hadi ‘Seduce Me’, hakuna namna utaishia kuupenda tu muziki wa Ali Kiba.

Sauti yake inaburudisha huku ikigharamia maisha yake, ikimjengea majumba makubwa na mwisho kumnunulia magari ‘makali’. Kwasasa Kiba anaendesha BMW X5.

 

6. AY


Kama ilivyo kwa Lady Jaydee, AY pia anabakia kuwa mmoja wa wakongwe wa Bongo Flavour wasiochuja.

Kutokea ‘Yule’ hadi ‘Zigo’, bila shaka AY bado yupo yupo sana kwenye ‘game’. Na kama ulikuwa unajiuliza anasukuma ‘ndinga’ gani, basi tarajia kukutananae ndani ya Range Rover Sport ya kijivu.

 

CHANZO: Mtandao wa Zoom

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *