Burudani

+VIDEO: Magufuli ‘amfungulia’ mlango Babu Seya

on

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amemtaka msanii Nguza Viking ‘Babu Seya’ na wanae kusahau kila kitu na kuanza kupiga kazi tu.
Disemba 9 mwaka huu, Magufuli aliwaachia huru Babu Seya na mwanae Papii waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha katika gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Ikulu Jijini Dar es Salaam leo baada ya familia hiyo kumtembelea kwa lengo la kumshukuru kwa kuwaachia huru, Rais aliwataka kupiga kazi kwa kuwa wako huru kwa sasa.
“Sikutegemea kama mtakuja, niliyoyafanya sio mimi ni mipango ya Mungu, nimetimiza wajibu wangu, niwatakie maisha mema, yaliyopita si ndwele tugange yajayo, endeleeni kufanya kazi, na mumtegemee sana Mungu,”alisema.
Kwa upande wake Babu Seya alimshukuru Rais kwa moyo wake, huku akiahidi kutomuangusha kwa kuwa kamruhusu kwenda kupiga kazi hivyo atatangaza hivi karibuni ratiba yake ya kazi.
“Yaani sijui niseme nini, nina furaha sana, nilikuwa naomba sana nikutane nae, najua mimi bado ni mwanamuziki nafurahi sana, sasa ni kuchapa kazi tu, hapa kazi tu,”alisema.
Kwa upande wake Papii alisema, wako katika mipango ya kutoa ngoma mpya kwani wamerejea kuuokoa muziki wa dansi, hivyo mashabiki wao wakae mkao wa kula.
Babu Seya aliongozana na watoto wake Papii Kocha pamoja na wanafamilia wengine Nguza Mbagu na Francis Nguza.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *