Kitaifa

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu Beno Kakolanya

on

JINA la kipa Beno Kakolanya lilianza kung’ara alipokuwa akiidakia Prisons ya Mbeya hadi mabingwa watetezi wa ligu kuu, Yanga walipomnunua mwanzoni mwa msimu uliopita.

Kabla ya hapo na hata sasa kuna mambo kadhaa yanaendelea katika maisha ya kipa huyo ambayo si wengi wanayafahamu, BOIPLUS imekukusanyia mambo 10 yasiyofahamika sana kuhusu maisha yake;

1. Ni shabiki mkubwa wa Barcelona ya nchini Hispania.

Juma Kaseja

2. Anamkubali sana kipa Juma Kaseja wa Kagera Sugar lakini ajabu hajawahi kukutana nae na kupiga stori zaidi ya uwanjani wakikutana kwenye mechi.

3. Barani Ulaya kipa anayemkubali sana ni Iker Casillas.

4. Ni shabiki mkubwa wa mazoezi ya viungo ambapo amekuwa akiendelea na mazoezi hata akiwa nyumbani kwake ambako mara nyingi hufanya mazoezi ya tumbo na kuruka kamba.

5. Starehe yake kubwa ni kutazama filamu za ngumi za nje, aliacha kutazama Bongo Movie mara baada ya Steven Kanumba kufariki dunia.

6. Ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Jenala.

Mama mzazi wa Beno, Eva Mwankusye

7. Anampenda mama yake Eva Mwankusye kuliko kitu kingine chochote.

8. Msimu wake wa kwanza kucheza ligi kuu (2013/14) alifungwa mabao matano katika mechi moja timu yake ya Prisons ilipokutana na Yanga kwenye dimba la Taifa.

9. Kipindi cha likizo ndefu humkuti sehemu nyingine zaidi ya jijini Mbeya kwenye ‘akademi’ iliyomlea iitwayo Mbaspo ambayo inamilikiwa na meneja wake Seleman Haroub.

10. Beno anamudu kutumia vizuri zaidi mguu wa kushoto kuliko anavyotumia wa kulia.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *