Kitaifa

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Edward Christopher ‘Edo’

on

LEO katika safu hii tupo na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Edward Christopher ‘Edo’ akifunguka mambo 10 ambayo mashabiki wengi wa soka hawayafahamu vizuri

1. Edo hana kipaji kingine chochote zaidi ya kucheza soka ambalo ndio ajira yake.

2. Kwenye muziki wa Bongo Flava siku hizi kuna ushindani mkali kati ya Abdul Nassib ‘Diamond Platnumz’ na Ali Kiba hadi kufikia hatua ya mashabiki kugawana ‘Team Mond’ na ‘Team Kiba’. Edo yeye ameweka wazi kuwa ni Team Mond.

3. Straika huyo wa zamani wa Simba hajaoa lakini ana mchumba ambaye anatarajia kufunga nae ndoa ili apate mtoto na kuitwa baba sasa.

4. Katika maisha yake ya mpira amekutana na makocha wengi lakini hajaona kama Seleman Matola aliyemkuza akiwa Simba B na Meck Mexime anayemfundisha sasa.

5. Siku ya furaha ambayo Edo hawezi kuisahau ni alipoibuka mfungaji bora wa kombe la BancABC ‘Super8’ akiifungia Simba mabao manane na kuipa ubingwa. Siku yake huzuni ni ile aliyopigiwa simu usiku akiwa amelala akipewa taarifa za msiba wa mama yake mzazi 2015.

6. Washambuliaji anaowakubali sana ni Emmanuel Okwi wa Simba na Neymar Jr anayekipiga na PSG ya Ufaransa.

7. Edo ni shabiki mkubwa wa timu ya Barcelona ya Hispania na Arsenal ya Uingereza huku akizihusudu sana timu za taifa za Brazil na Nigeria.

8. Straika huyo anatamani sana kucheza soka nje ya Tanzania hasa nchini Afrika Kusini.

9. Hakuna kitu anachotamani zaidi kama kukutana na wachezaji aliocheza nao Simba B ili wacheze tena timu moja.

10 Kikosi chake bora ni kile alichokua nacho kwenye michuano ya Super8 ambacho ni;

KIKOSI CHA KWANZA
1. Abuu Magube
2. Wiliam Lucian ‘Gallas’
3. Emil Mugeta
4. Hassan Isihaka
5. Hassan Hatibu
6. Abdala Seseme
7. Haruna Chanongo
8. Saidi Ndemla
9. Rashid Mkoko
10. Edward Christopher
11. Ramadhani Singano

WACHEZAJI WA AKIBA
1. Saleh Malande
2. Omari Waziri
3. Ibrahim Ajib
4. Jamal Mwambeleko

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

1 Comment

  1. Dickson Masanja

    December 6, 2017 at 9:52 am

    Hongera sana Akram Msangi ‘Mido’ hizi ndio kazi sasa, story nzuri ni lazima uipambanie uumize kichwa na uwekeze muda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *