Kitaifa

Manji aachiwa huru kesi ya madawa ya kulevya

on

MFANYABIASHARA Yusuf Manji ameachiwa huru katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuithibitishia Mahakama kama kweli alikuwa anatumia madawa hayo.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Cyprian Mkeha ilichukua saa moja kabla ya kuachiwa huru kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa mabingwa wa ligi kuu ya Vofacom, klabu ya Yanga.

Hakimu Mkeha alisema ni kweli mkojo wa Manji ulipimwa katika ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali mwezi Februari na kukutwa na viashiria vya dawa za kulevya lakini upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kwakua vinaweza kupatikana kwa namna nyingine pia sio kwa dawa za kulevya pekee.

“Upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kuwa mtuhumiwa alitumia madawa ya kulevya kwakua viashiria vilivyopatikana kwenye mkojo wake vinaweza kupatikana kwa njia nyingine,” alisema Mkeha.

Kwa upande wake Wakili wa mfanyabiashara huyo Hajra Mvula alisema kuwa baada ya kufanikiwa kushinda kesi hiyo watakaa chini na kujua wafanye nini kuhusu suala hilo.

Katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kuliwepo na wanachama na mashabiki wa Yanga wakiongozwa na Katibu mkuu Boniface Mkwasa ambaye alishukuru kuachiwa huru kwa Mwenyekiti huyo.

“Mimi ndiye nilimuwekea dhamana kwenye kesi hii, tunamshukuru Mungu tumemaliza salama jambo hili sasa tuangalie mambo gani yatafuata mbeleni,” alisema Mkwasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *