Afrika

Mashabiki waitosa Benin ikilazimishwa sare na Stars

on

MATOKEO ya mechi tatu za mwisho kabla ya kupambana na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ yanaweza kuwa ndio sababu ya mashabiki wa Benin kutojitokeza kwa wingi uwanjani kuishuhudia timu yao ikilazimishwa sare ya bao moja leo.

Stars imepata sare hiyo muhimu ugenini baada ya Elius Maguli kusawazisha bao la kipindi cha kwanza la nahodha wa Benin, Stephan Sessegnon alilolifunga kwa njia ya penati tata dakika 30.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa umemalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja Stade de l’Amitie wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 lakini mashabiki wa nchi hiyo walishindwa kujaza japo nusu ya uwanja huku taarifa zikisema ni 15,000 pekee ndio walikata tiketi.

Wachezaji wa Taifa Stars

Timu hiyo imeshindwa kupata matokeo mazuri katika michezo mitatu ya hivi karibuni ambapo kabla ya mchezo wa leo ililazimishwa sare mbili na kushinda moja kwenye uwanja huo wa nyumbani.

Matokeo ya sare kwa Stars iliyoonesha nidhamu ya hali ya juu leo ni mazuri na yanayoweza kuipandisha kwenye viwango vya FIFA hasa kwavile ni ugenini.

Haya hapa ni mabao yote mawili katika mchezo huo:

Goli la Stephan Sessegnon

 

Goli la Elius Maguli

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *