Kitaifa

Matawi Simba, Yanga yavimbiana Kurasini

on

TIMU za soka za matawi ya klabu kongwe za Simba na Yanga, Simba Damu Fans (SDF) na Yanga Facebook Fans (YFF) zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwenye uwanja Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam jioni ya l.

SDF ilikuwa ya kwanza kugusa nyavu za wapinzani wao ikiwa ni dakika 17 tu tangu kuanza kwa pambano hilo baada ya straika wao Mbwana Masaninga kuwachambua mabeki pamoja na kipa wa YFF kabla hajatupia nyavuni kiulaini.

Kilosi cha Simba Damu Fans

SDF waliendelea kutawala mchezo huo wakifanya mashambulizi kadhaa ambapo dakika chache baadae walinzi wa YFF walishindwa kumzuia winga Gasper Gabriel aliyewapatia Wekundu hao wa Tabata Kimanga bao la pili akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Godfrey aliyepokea pasi toka kwa kiungo wao Arnold.

Kipindi cha pili YFF walifanya mabadiliko kadhaa yaliyoifufua timu
hiyo na kuanzisha ‘msako’ langoni mwa SDF ambapo dakika ya 68, Osama Haji aliipatia bao la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo umbali wa takribani mita 30 toka langoni.

Kikosi cha Yanga Facebook Fans

Ikionekana kama vile pambano hilo lingemalizika kwa SDF kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya majirani zao hao wa Tabata, YFF walitumia tena mpira wa adhabu ndogo kusawazisha zikiwa zimesalia dakika mbili tu mwamuzi amalize mechi.

Michezo hiyo ya kirafiki imekuwa ikianzisha na kudumisha mahusiano mazuri baina ya mashabiki na wanachama wa timu hizo zenye upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja.

 

 

Kutazama video za matukio mbalimbali ya MICHEZO na BURUDANI tafadhali SUBSCRIBE kwenye chaneli yetu ya YouTube kwa jina la BOIPLUS TV. Bofya picha hii hapa chini itakupeleka mara moja…

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *