Kimataifa

Mbali na George Weah, wanasoka hawa pia walitisha kwenye Siasa

on

JANUARI 22, nchi ya Liberia iliweka historia pale mwanasoka nguli na mwafrika pekee kuwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or, George Weah alipoapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.

Weah anakuwa mwanasoka wa kwanza duniani kushika nyadhifa kubwa zaidi serikalini hiyo ikiwa ni baada ya kupambana kwa kipindi kirefu.

Lakini mbali na Weah kuna wasakata kabumbu kadhaa waliwahi kutisha kwenye medani ya siasa na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali za kiserikali.

Romario
Huyu ni mchezaji wa zamani wa Brazil na klabu za PSV, Barcelona na Flamengo, aliingia rasmi kwenye siasa 2010 na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa ‘Chamber of Deputies’.

Romario alitumia nafasi hiyo kuisadia Brazil kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2014 na baadaye akachaguliwa kuwa seneta wa jimbo la Rio de Janeiro na kuweka rekodi ya kupata ushindi wa kura nyingi kuliko mtu yeyote jimboni hapo.

 

Gianni Rivera
Gianni ni mmoja wa wachezaji waliocheza michezo mingi zaidi katika klabu AC Milan, nyuma ya Paolo Maldini, Franco Baresi na Alessandro Costacurta akishuka dimbani katika mechi 658 kati ya mwaka 1960 na 1979.

Baada ya kustaafu soka alikuwa makamu wa Rais wa klabu hiyo na baade kuingia kwenye Siasa.

1986 alichaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama cha ‘Christian Democracy Party’ na baadae kuwa katika wizara ya ulinzi.

2005 alichaguliwa kuwa mbunge wa umoja wa ulaya ‘Member of European Parliament’

 

Kakha Kaladze
Mlinzi wa zamani wa Ac Milan aliyestaafu soka 2012 na kuingia kwenye siasa alijiunga na chama cha Democratic Georgia Party na Oktoba mwaka huo huo akachaguliwa kuwa mbunge.

Mshindi huyo mara mbili wa ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA), baada ya kushinda ubunge aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu na baadae waziri wa Nishati.

 

Andriy Shevchenko
Straika machachari wa klabu za Dynamo Kyiv, Ac Milan na Chelsea kuanzia 2006 hadi 2009.

2012 alistaafu soka na kuingia kwenye siasa kupitia chama cha Ukraine Forward Party japo hakupata mafanikio katika siasa na kuachana nazo.

 

Titi Camara
Straika wa zamani wa Lens, Liverpool na West Ham ambaye muda wake mwingi wa soka ameutumia katika ligi kuu ya Uingereza na Ufaransa na baadae kurudi nchini kwake Guinea.

Camara amekuwa katika benchi la ufundi la timu ya Taifa na baadae kuwa kocha wa timu ya taifa ya Guinea 2009.

Baada ya hapo akateuliwa kuwa waziri  wa michezo  baada ya uchaguzi ambao Rais  Alpha Conde aliibuka mshindi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *