Kitaifa

Mbao wakishangaa tu Simba wameivuruga Mtibwa

on

TIMU ya Simba ina nafasi kubwa ya kuharibu hesabu za Mtibwa kwa kuiondoa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom endapo itashinda kesho katika mchezo dhidi ya Mbao FC utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo huo ulikuwa ufanyike siku ya Jumamosi kama michezo mingine lakini kutokana na uwanja huo kuwa na matumizi mengine siku hiyo umerudishwa nyuma hadi kesho ambapo Mbao wasipojipanga watageuzwa ngazi.

Simba ambayo kwa sasa ina pointi saba ikiibuka na ushindi kwenye mchezo huo itafikisha alama 10 na kuishusha kileleni Mtibwa Sugar yenye pointi tisa ikiwa imecheza mechi tatu.

Viungo Haruna Niyonzima na Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’ wanatajwa kuwa miongoni mwa nyota wa Simba watakaoshuka dimbani kesho baada ya hali zao za afya kutengemaa.

Kikosi cha Mtibwa kinachoongoza ligi

Jumamosi kutakuwa na michezo minne ambapo mabingwa watetezi Yanga watacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Singida United itaialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui FC mchezo utaofanyika uwanja wa Mwadui Complex huku Majimaji ikiikaribisha Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Jumapili Septemba 24 kutakuwa na michezo mitatu ambapo Ruvu Shooting itacheza na vinara Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Mchezo wa mwisho siku hiyo utafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex kati ya wenyeji Azam FC dhidi ya Lipuli FC kutoka mkoani Iringa na kukamilisha mzunguko wa nne wa timu zote 16.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *