Kitaifa

MBONDE + Video: Tulieni, hiyo 3-5-2 ikikolea moto Simba mtaipenda

on

BEKI kisiki wa Wekundu wa Msimbazi Simba, Salim Mbonde amepata habari kuwa kocha Masoud Djuma anatumia mfumo mpya wa 3-5-2 kisha akasema “hiyo imekaa poa sana, vuteni subra”.

Mbonde aliyesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro ameiambia BOIPLUS anaupenda mfumo huo huku akiwatonya mashabiki wa Wekundu hao kuwa wavumilie tu huku mwanzoni ila ukizoeleka Mnyama atatisha.

“Nimeona mfumo mpya wa mwalimu, kiukweli ni mzuri sana nawaomba mashabiki wawe na subra ukizoeleka watafurahi sana kwasababu ni mfumo wa ushindi kwani timu inashambulia muda wote.

Salim Mbonde akifanya mazoezi Gym

“Lakini pia una madhara kidogo kama wachezaji watashindwa kuelewana na wengine kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hii ni kwasababu nyuma wanakua watu wachache lakini Simba ina wachezaji wazuri kila idara kwahiyo hakuna kitakachoharibika,” alisema Mbonde.

Beki huyo ambaye yupo Morogoro amekiri pia kuwa anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya ‘Gym’ baada ya kupona jeraha la goti aliloumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimeanza mazoezi ya Gym, wiki ijayo natarajia kuanza mazoezi ya ufukweni na siku si nyingi nitarudi uwanjani kuanza kuitumikia timu yangu.” ali sema.

Mbonde alimaliza kwa kuwaomba mashabiki wa Simba waendelee kumuombea azidi kuimarika haraka ili aweze arudi kuitumikia timu yake kwani anatambua ana deni kubwa kwao kutokana na imani kubwa waliyonayo kwake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *