Burudani

Mchekeshaji Joti alivyochukua ‘jiko’

on

HARUSI ya mchekeshaji Lucas Mhavile ‘Joti’ na mchumba wake wa miaka mingi Tumaini ilifungwa jana ambapo sherehe ya harusi hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Harusi hiyo ilikusanya watu mbalimbali maarufu wakiwemo wasanii wenzake wa kundi la Comedy wakiongozwa na Mpoki, Wakuvanga, Mack Regan pamoja na Seki ambaye alikuwa ndiye ‘Best Man’ wa Bwana Harusi.

Pamoja na burudani ambazo zilitolewa huku maharusi hao wakiwa na furaha kubwa ya kutimiza tendo hilo kubwa na takatifu kwa Mwenyezi Mungu ‘funika bovu’ ilikuwa ni baada ya mtoto wao kusimama na kuimba wimbo uliohusu upendo kwa wazazi wake ambapo ukumbi mzima ulionekana kupooza kwa hisia kali za majonzi.

Majanzo hayo yalitokana na jinsi binti huyo wa Joti na Tumaini alivyoonyesha hisia kali wakati akiwaimbia wazazi wake wimbo huo hali iliyopelekea hata mama yake kutokwa na machozi huku wageni waalikwa wakimtunza binti huyo. Wimbo huo ulikuwa ni wa kuwatakia kheri wazazi wake katika ndoa yao na kwamba waishi kwa upendo na amani pasipo kutengena.

Burudani nyingine mbali ya kundi la Comedy ambao ndio walikuwa wa mwisho kuingia ukumbini baada ya maharusi kuingia ilitolewa na msanii wa muziki wa dansi Christian Bela aliyeimba nyimbo tatu mfululizo ukiwemo wimbo wake wa Nani kama Mama.

Ulinzi kwa maharusi hao ulikuwa mkubwa hasa pale ambapo kila mmoja akitaka kucheza na maharusi jambo ambalo lilihofiwa kuleta usumbufu kwa wanandoa lakini mshehereshaji Ephraem Kibonde alifanikiwa kudhibiti hilo na kuwaacha wanandoa hao wakicheza kwa kujinafasi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *